
Hatua hiyo itauwezesha Umoja wa Ulaya kuondokana na utegemezi ambao umekuwa ukijaribu kukomesha bila mafanikio licha ya vita vya Urusi nchini Ukraine.
Katika mkutano wao huko Luxembourg, mawaziri hao waliidhinisha mpango wa halmashauri kuu ya umoja huo kufunga bomba la kuagiza gesi kutoka Urusi na sasa wanasubiri bunge la Ulaya kuafiki uamuzi huo.
Lars Aagaard ambaye ni Waziri wa nishati wa Denmark ametaja hatua hiyo kuwa muhimu kuifanya Ulaya kuweza kujitegemea kivyake kinishati.
Mpango huo ni sehemu ya mkakati mpana wa Umoja wa Ulaya kuachana na nishati ya Urusi.