Gavana wa chama cha Democratic huko California amekosoa maonyesho ya kijeshi ya Trump ambayo yalisababisha kufungwa barabara kuu, akiyataja kuwa ni ishara ya Rais kutanguliza mbele “kiburi kuliko uwajibikaji.”

Gavana Gavin Newsom wa California amesema katika taarifa kwamba utunishaji misuli wa kijeshi wa Trump, ambao umejumuisha ufyatuaji wa risasi za mizinga kwenye barabara kuu karibu na Camp Pendleton, ulikuwa “onyesho la kipuuzi, hatari na lisilo la lazima.”

“Kutumia jeshi kuwatisha wapinzani sio nguvu, ni uzembe,” ameongeza Gavin Newsom.

Newsom iliwataka waandamanaji kuyatambua maandamano hayo kama “tangazo la uhuru dhidi ya dhuluma na ukandamizaji.”

Ukosoaji dhidi ya Trump umekuja wakati shughuli hiyo ya kutunisha misuli ya kijeshi iliambatana na maandamano ya kitaifa ya “Hapana kwa Ufalme” (No Kings).

Watu milioni saba kote Marekani walishiriki katika maandamano ya pili ya “No Kings” dhidi ya Rais Donald Trump, yakisajiliwa kama maandamano makubwa zaidi ya siku moja dhidi ya rais aliyeko madarakani katika historia ya sasa ya nchi hiyo.

Mamilioni ya waandamanaji walijiunga na maandamano katika maeneo na miji zaidi ya 2,500 katika majimbo yote 50, na miji kadhaa ya mataifa mengine, kupinga kile waandaaji wameelezea kama “unyakuzi wa mamlaka wa Trump.”

Maandamano hayo yanaashiria mvutano unaoongezeka kati ya Ikulu ya White House na serikali za jimbo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *