
Wahanga hao wamesema hayo, siku chache tu baada ya Tume ya Vatican ya kuwalinda Watoto kuwashutumu viongozi wa ngazi ya juu kanisani humo kulegea kuwasaidia wahanga.
Papa Leo alikutana na muungano wa kimataifa wa kukomesha manyanyaso ya Watoto mikononi mwa makasisi pamoja na wahanga wanne wa dhuluma hizo.
Kwa miongo mingi, kanisa Katoliki lenye takriban waumini bilioni 1.4 ulimwenguni kote limetikiswa na kadhia ya kuficha uovu huo, hali ambayo inachafua jina na sifa ya kanisa mbali na hasara ya mamilioni ya dola kulipa fidia.
Wahanga wamesema, Papa Leo alikuwa mkaribu kwao na aliwasikiliza kwa makini. Wamemtaka Papa Leo kutunga sheria itakayokomesha kabisa manyanyaso hayo kanisani ulimwenguni.