
Tim Law, muanzilishi mwenza wa taasisi ya Ending Clergy Abuse (ECA), iliyoko Marekani iliyo na lengo la kusitisha unyanyasaji unaodaiwa kufanywa na makasisi amesema, nia hasa ya mkutano huo ni kuwa na uhusiano mwema na Papa Leo na kupata hakikisho lake la kujadili masuala haya kwa uwazi. Amesema Papa ameridhia matakwa yao.
Tim ameongeza kuwa mkutano huo uliowahusisha pia mawakili wanaowawakilisha wahanga hao kutoka zaidi ya mataifa 30 ulipaswa kufanyika kwa dakika 20 tu lakini ulirefushwa hadi saa moja.
Kundi hilo limemtaka Papa Leo kuweka sheria ya kutovumilia unyanyasaji na kukomesha kabisa dhuluma hiyo. Amesema tayari sheria hiyo inafanya kazi nchini Marekani kwa makanisa yote. makanisani. ambayo tayari imewekwa nchini Marekani kwa
Chini ya sheria iliyoundwa na maaskofu wa Marekani, kasisi anapaswa kuondolewa kikamilifu kutoka katika huduma za kikanisa iwapo kisa chochote cha unyanyasaji wa kingono wa watoto chini ya miaka 18 kitakachothibitishwa dhidi yake.
Wahanga hao wamesema hayo, siku chache tu baada ya Tume ya Vatican ya kuwalinda Watoto kuwashutumu viongozi wa ngazi ya juu kanisani humo kulegea kuwasaidia wahanga. Kwa miongo mingi, kanisa Katoliki lenye takriban waumini bilioni 1.4 ulimwenguni kote limetikiswa na kadhia ya kuficha uovu huo, hali ambayo inachafua jina na sifa ya kanisa mbali na hasara ya mamilioni ya dola kulipa fidia.
ECA had written to Pope Leo to ask for a meeting after his election as head of the world’s 1.4 billion Catholics in May.
Law described it as a “big step”, “historic” and “amazing”. The Vatican confirmed that Pope Leo had an audience the ECA without saying what was discussed.