Ripoti rasmi zinasema, mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel yameharibu asilimia 97 ya shule za Ukanda wa Gaza na hivyo kuhatarisha mustakbali wa kielimu wa wanafunzi laki tatu wa Kipalestina.

Uchunguzi unaonyesha kuwa tangu kuanza kwa mashambulizi ya kijeshi ya Israel huko Gaza mnamo Oktoba 2023, mfumo wa elimu katika eneo hilo umepatwa na maafa ambayo hayajawahi kutokea.

Wizara ya Elimu ya Palestina imetangaza kuwa shule 172 za umma zimebomolewa kabisa na zingine 118 zimeharibiwa. Zaidi ya hayo, zaidi ya shule 100 zinazosimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) pia zimeharibiwa vibaya.

Shule za UNRWA, Gaza

Ripoti zinsema: Athari mbaya za uharibifu huu kwa maisha ya wanafunzi haziwezi kufikirika. Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 12 kutoka Khan Yunis anasema: “Imekuwa miaka miwili tangu nilipoketi katika darasa halisi. Vitabu vyangu vimechomwa moto na baadhi ya marafiki zangu wameuawa.”

Mwanafunzi huyo ambaye kwa sasa anaishi na familia yake katika makazi yenye watu wengi, anaongeza: “Hasara mbaya zaidi ni elimu yangu kwa sababu ina maana ya kupoteza maisha yangu ya baadaye.”

Takwimu za maafa ya binadamu yaliyosababishwa na mashambulizi ya Israel dhidi ya watu wa Gaza, zinatajwa kuwa za kutisha sana. Wanafunzi 17,711 wameuawa, 25,897 wamejeruhiwa, na walimu 763 wameuawa katika mashambulizi ya kikatili ya Isarel. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *