Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 424.6 kwa ajili ya miradi ya maendeleo mkoani Rukwa, ikiwemo ukarabati wa uwanja wa ndege wa Sumbawanga, ujenzi wa barabara za lami na kazi za matengenezo.

Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Mgeni Mwanga, amesema miradi hiyo inalenga kuboresha usafiri na kuimarisha shughuli za kiuchumi katika mkoa huo.

Mkoa wa Rukwa una mtandao wa barabara wa kilometa 1,250.84, ambapo barabara kuu ni kilometa 415.86 na za mkoa ni kilometa 834.98.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *