Messi

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 38, anatarajiwa kusaini mkataba mpya na klabu ya soka ya Marekani Inter Miami. (Fabrizio Romano)

Arsenal na Tottenham ni miongoni mwa vilabu vya Ligi ya Premia vinavyomfukuzia mshambuliaji wa Saint-Etienne Mfaransa mwenye umri wa miaka 17 Djylian N’Guessan. (Caught offside)

Kiungo wa kati wa Getafe Mhispania Luis Milla, 31, amevutia macho ya meneja wa Aston Villa Unai Emery na mkufunzi wa Atletico Madrid Diego Simeone msimu huu. (Fichajes – kwa Kihispania)

Chelsea wako tayari kutoa zaidi ya euro 100m (£87m) kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Samuel Omorodion mwenye umri wa miaka 21 kutoka Porto msimu ujao. (Fichajes – kwa Kihispania)

Wachezaji wa zamani wa Manchester United Eric Cantona, Wayne Rooney na David Beckham wameombwa kuwasilisha ombi la kuinunua klabu hiyo na muungano wa kibiashara usiojulikana kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu. (Guardian)

Wasaka vipaji au wa klabu ya Barcelona walikuwa wakimfuatilia mshambuliaji wa zamani wa Uingereza Mason Greenwood, 21, wakati alipoifungia Marseille mabao manne wikendi hii. (TBR Football)

Samuel Omorodion

Chanzo cha picha, Getty Images

Meneja wa Fulham Marco Silva ndiye chaguo la kwanza la Nottingham Forest kuchukua nafasi ya Ange Postecoglou, lakini anasita kuondoka Craven Cottage katikati ya msimu. (Times – usajili unahitajika)

Bournemouth inajiandaa kupokea ofa kutoka kwa vilabu vinavyotaka kuksajili mshambuliaji wa Ghana Antoine Semenyo, 25, katika dirisha la uhamisho la baadaye. (Football Insider)

Klabu za Newcastle na Aston Villa zinapigiwa upatu kumsajili mlinzi wa Ecuador Joel Ordonez, 21, kutoka Club Brugge. (Caught Offside)

Casemiro anatarajiwa kupewa kandarasi mpya katika klabu ya Manchester United lakini mkataba wowote utahitaji kiungo huyo wa kati wa Brazil, 33, kukatwa mshahara mkubwa. (Football Insider),

Nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes anafikiria kuhama klabu mwishoni mwa msimu huu ikiwa hawataimarika. Bayern Munich wana nia ya kumsajili kiungo huyo wa kati wa Ureno mwenye umri wa miaka 31. (Fichajes – kwa Kihispania)

Pia unaweza kusoma:

Imetafsiriwa na mbia Hirsi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *