Hayo yalijiri siku ya Ijumaa wakati wa mkutano uliokumbwa na mvutano na ambao uliuvunja moyo ujumbe wa Ukraine. Hayo ni kulingana na vyanzo vilivyofahamishwa kuhusu matokeo ya mkutano huo na kuongeza kuwa Zelensky hakubaliani na shinikizo hilo.

Urusi ilinyakua baadhi ya maeneo ya Ukraine ikiwemo Lohansk na Donetsk na Putin anataka Ukraine kusalimisha maeneo hayo.

Trump pia alikataa kuipa Ukraine makombora aina ya Tomahawk akisema Marekani inayahitaji makombora hayo na asingependa nchi yake iwe hatarini kwa kupungukiwa zana hizo.

Baada ya mkutano wake na Zelensky, Trump alitoa wito wa usitishaji mapigano katika maeneo yanakoshuhudiwa vita kwa sasa, kati ya Urusi na Ukraine.

Mzozo wa Urusi na Ukraine ulianza Februari mwaka 2022 wakati Urusi ilipoivamia Ukraine kijeshi.

Mawaziri wa EU wakutana kujadili mizozo ya Ukraine na Mashariki ya Kati

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana Jumattau huko Luxembourg, kujadili mizozo ya Mashariki ya Kati na Ukraine.

Ukraine Lviv 2025 | Mkutano wa Ukraine-EU huko Lviv
Mawaziri wa Umoja wa Ulaya kutafuta ufumbuzi wa fumbo la mzozo wa Urusi na UkrainePicha: Roman Baluk/REUTERS

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii Sybiha pia atajiunga na mawaziri hao kuainisha hali ilivyo katika maeneo ya mapambano yanayohitaji misaada ya dharura, na pia kutoa taarifa kuhusu juhudi za kidiplomasia za hivi karibuni za Marekani.

Mkutano huo unajiri siku chache tu baada ya Rais Donald Trump kutangaza kuwa atakutana na Putin katika mji mkuu wa Ugiriki- Budapest.

Mkutano unaopangwa wa Putin katika nchi ya Umoja wa Ulaya umeshutumiwa vikali. Kestutis Budrys ambaye ni waziri wa Mambo ya Nje wa Lithuania amesema:

“Hakuna mahali pa wahalifu wa vita barani Ulaya. Hakuna njia kupitia Ulaya kwa kwa wahalifu wa vita kwenda kwenye tukio lolote. Hili ni jambo muhimu kwetu kusisitiza tena. Tuko imara katika kuiunga mkono Ukraine na tunaendelea na shinikizo letu dhidi ya Urusi.”

Mawaziri hao pia watajadili mapendekezo ya umoja huo ya kutumia mabilioni ya yuro kutokana na mali zilizozuiwa za Urusi kulipa mikopo kwa Ukraine.

Mkutano wa Jumatatu ni wa kwanza wa mawaziri hao tangu kuanza kutekelezwa kwa makubaliano ya usitishaji vita huko Ukanda wa Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *