Katika mechi za mwishoni mwa wiki, wachezaji kutoka vilabu mbalimbali walionyesha mshikamano dhidi ya mpango huo wa kibiashara ambao unalenga kuhamisha mechi moja ya La Liga nje ya Uhispania.

Kwa mujibu wa viongozi wa La Liga, mpango huo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kuongeza mapato ya ligi kupitia mauzo ya tiketi, bidhaa rasmi na ushirikiano wa kibiashara na kampuni za Marekani.

Hatua hiyo ya wachezaji imechukuliwa kama njia ya kuonyesha kutoridhishwa na mpango huo ambao umeibua maswali kuhusu maslahi ya wachezaji, mashabiki na utamaduni wa soka nchini humo.

Kocha wa Barcelona, Hansi Flick, amesema wazi kuwa yeye na wachezaji wake hawafurahii kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita 7,000 kwenda kucheza mechi ya kawaida ya ligi nchini Marekani.

Vilabu vilivyoshiriki maandamano hayo ya kimya kimya:

– Barcelona vs Girona

– Atletico Madrid vs Osasuna

– Sevilla vs Mallorca

– Villarreal vs Real Betis

– Oviedo vs Espanyol (Ijumaa jioni – waliweka mfano wa kwanza)

Katika mechi hizo, wachezaji walibaki wamesimama kwa sekunde 15 za mwanzo, wakitoa ujumbe wa wazi wa kupinga uamuzi wa La Liga japo bila ya kuathiri mchezo moja kwa moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *