
Huku msaada wa kibinadamu unaohitajika ukisalia kuwa haba huko Gaza, waanchi wa Misri wametaka kufunguliwa tena kivuko cha mpakani cha Rafah kwa ajili ya kuingiza misaada neo la Ukanda wa Gaza.
Wananchi wa Misri wametoa wito huo huku jeshi la Israel likithibitisha kufanya mashambulizi ya anga katika mji huo wa Palestina unaopakana na Misri.
Israel ilipanga kukifungua tena kivuko cha Rafah Jumatano iliyopita kama sehemu ya awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa kati ya utawala huo na harakati ya Hamas.
Wamisri katika mji mkuu wa nchi hiyo, Cairo, wameeleza mshikamano wao na watu wa Palestina wa Ukanda wa Gaza wakisema kuwa kufunguliwa tena kivuko muhimu cha Rafah kwa ajili ya kupitisha misaada ya kibinadamu kutaokoa maisha ya watu wengi.
“Haya ni matakwa ya Wamisri wote kwa miaka miwili iliyopita. Tunasisitiza kufunguliwa tena vivuko cha Rafah. Tunataka misaada ya kibinadamu iingie Gaza na tungependa mgogoro huu wa binadamu umalizike,” amesema mkazi wa Cairo kwa jina la Jada.
Israel, juzi Jumamosi, ilisema kuwa kivuko cha Rafah kinachopatika kati ya Misri na Gaza kitaendelea kufungwa hadi itakapotolewa taarifa mpya.
Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu alisema kuwa kufunguliwa kivuko hicho kunategemea iwapo Hamas itaikabidhi Israel miili ya mateka wake walioaga dunia.