Kemikali hii ambayo inaitwa antifreeze ambayo hutumika hasa kupunguza kiwango cha kuganda kwa maji katika mashine kama injini za magari ni hatari kwa sababu inaweza kusababisha kushindwa kwa figo kwa haraka ikitumika kwa binaadamu. Vifo hivi vimetokea ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, na vimesababisha hasira na huzuni miongoni mwa jamii ya wananchi wa India.

Mwaka 2023, watoto 18 walifariki dunia nchini Uzbekistan baada ya kutumia dawa ya kikohozi iliyotengenezwa India. Mwaka 2022, takriban watoto 70 walipoteza maisha nchini Gambia kwa sababu ya matumizi ya dawa hio. Katika jimbo la Jammu nchini India, watoto 12 walifariki kati ya mwaka 2019 na 2020 kutokana na dawa yenye kilainishi cha DEG.

Shirika la Kudhibiti Dawa la India pamoja na maafisa wa majimbo na mashirika mengine ya udhibiti, walichukua hatua haraka ikiwemo ile ya kuzuia uuzaji wa dawa zenye kemikali hizo.

Indien, Nadia | Mahali kunakohifadhiwa dawa
Soko la dawa nchini India linakadiriwa kuwa na thamani ya takriban dola bilioni 50 huku nchi hio ikiwa ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa dawa duniani.Picha: Prajit Bhadra

Dr Gahane ni Afisa wa Shirika la Kudhibiti Dawa la India, amesema kuwa wameanzisha ukaguzi katika viwanda 19 vya dawa katika majimbo sita ili kubaini mapungufu ya ubora. Mmiliki wa kampuni ya Sresan Pharmaceuticals, iliyotengeneza dawa hiyo, amekamatwa na kampuni hiyo imefungwa rasmi.

Viwango vya udhibiti wa dawa vilitofautiana 

Hata hivyo, kila jimbo nchini India lina mamlaka yake ya kusimamia utengenezaji wa dawa, hali inayosababisha viwango vya udhibiti kutofautiana. Soumya Swaminathan, aliyekuwa mwanasayansi mkuu wa Shirika la Afya Duniani amesema kuwa mfumo wa udhibiti wa dawa nchini India unahitaji marekebisho makubwa huku akisema sekta hio pia inatawaliwa na  rushwa.

Tafiti za kisayansi zinaonyesha kuwa kati ya asilimia 20 hadi 25 ya dawa zinazopatikana sokoni nchini India hazifikii viwango vinavyotakiwa. Nakul Pasricha, Mkurugenzi Mtendaji wa PharmaSecure, amesema kuwa nchi inahitaji ufuatiliaji wa mara kwa mara na hatua kali dhidi ya wanaokiuka sheria.

Soko la dawa nchini India linakadiriwa kuwa na thamani ya takriban dola bilioni 50 huku nchi hio ikiwa ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa dawa duniani, na ni nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani.

Matukio haya yameibua wito wa dharura wa kufanyika marekebisho ya mfumo mzima wa usimamizi wa dawa nchini India. Wataalamu wanasisitiza kuwa bila mabadiliko ya haraka, maisha ya watu  hasa watoto  yataendelea kuwa hatarini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *