Klabu ya Yanga nchini Tanzania imeanza rasmi mchakato wa kumsaka kocha mkuu mpya baada ya kuvunja mkataba na Romain Folz, chini ya uongozi wa Rais Mhandisi Hersi Said.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka klabu ya Yanga SC, mkataba wa Romain Folz umevunjwa kwa makubaliano ya pande zote mbili kufuatia matokeo yasiyoridhisha, ikiwemo kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Silver Strikers ya Malawi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kipigo hicho kilikuwa cha kwanza kwa Yanga msimu huu na kilichochea uamuzi wa uongozi chini ya Rais Mhandisi Hersi Said kuanza mchakato wa mabadiliko ya benchi la ufundi.

Aliyekuwa kocha msaidizi, Patrick Mabedi, amekabidhibiwa jukumu la kuiongoza timu kwa muda akisubiri uteuzi rasmi wa kocha wa kudumu.

Hakuna jina lililotangazwa rasmi hadi sasa, lakini vyanzo vya habari vinaeleza kuwa majina kadhaa yanachunguzwa kwa kina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *