Shirika hilo limesema yote hayo yanafanyika kwa lengo la kueneza hofu na kudhibiti ushiriki wa raia kuelekea uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba, 2025. Taarifa hiyo inasema kuwa chini ya uongozi wa  Rais Samia Suluhu Hassan , matumaini ya mageuzi yameyeyuka, huku ukandamizaji ukiendelea kwa njia ya mashambulizi, kukamatwa kiholela, mauaji ya kiholela na watu kutoweka kwa nguvu bila yeyote kuwajibishwa.

Amnesty  pia imebaini ukiukwaji mkubwa na wa kimfumo wa haki za binadamu, ikiwemo mateso, unyanyasaji, na mauaji ya kiholela ya viongozi wa upinzani na wanaharakati.

Shirika hilo linazitaka mamlaka za Tanzania kusitisha kampeni ya ukandamizaji dhidi ya wapinzani, kufuta mara moja mashtaka ya uongo na yenye nia ya kisiasa dhidi ya wote waliokamatwa kwa sababu ya maoni yao ya kisiasa au kidini akiwemo kiongozi wa upinzani Tundu Lissu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *