Serikali ya Côte d’Ivoire na makao maku ya jeshi wanaripoti kwamba mwathiriwa-afisa ambaye amekuwa akiongoza kikosi cha askari-alifariki mapema asubuhi ya Jumatatu, Oktoba 20, wakati wa operesheni kwenye barabara ya Agboville-Grand Yapo-Azaguié. Mwathiriwa alipigwa risasi na “watu waliojifunika nyuso wakiwa wamejihami kwa bunduki” ambao “waliweka vizuizi” barabarani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Abidjan, Bineta Diagne

Askari huyo alifariki kusini mashariki mwa Côte d’Ivoire siku ya Jumatatu, Oktoba 20, kulingana na mamlaka huko Abidjan. Tukio hilo lilitokea mapema sana, karibu saa 10:00 alfajiri “. Watu waliojihami bunduki za kivita waliweka vizuizi” kwenye barabara kuu ya Agboville-Grand Yapo-Azaguié, serikali imesema katika taarifa, ambapo pia imebainisha kuwa mabasi kadhaa “yalizuiliwa na washambuliaji waliweza kuiba vitu kadhaa na pesa” kwenye barabara hiyo.

Kikosi cha askari kisha kiliingilia kati. Hata hivyo, katika eneo la tukio, “askari waliokuwa wakishikilia doria walipigwa risasi,” pia imesema taarifa hiyo. Afisa aliyekuwa anaongoza doria alifariki kutoana na majeraha aliyoyapata alipopigwa risasi.

Muda mfupi baadaye, watu walijaribu kuweka vizuizi katika baadhi ya vijiji karibu na Agboville, mkazi mmoja ameiambia RFI. Vizuizi hivi viliondolewa haraka na vikosi vya usalama, na utulivu ukarejea mchana, chanzo hicho kimeongeza.

Serikali inalaani “vitendo vya ukatili vilivyopangwa”

Ingawa hakuna aliyedai kuhusika na vitendo hivi, serikali, ambayo imejikita katika kulinda nchi wakati wa kipindi cha uchaguzi na kupiga marufuku maandamano kwa miezi miwili, imeshutumu “vitendo vya ghasia vilivyopangwa kutekelezwa kando ya maandamano ya hivi karibuni.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *