
Wajumbe kutoka DRC na Rwanda wanatarajia kukutana kuanzia leo Oktoba 21 na kesho Jumatano Oktoba 22 mjini Washington kwa kikao cha tatu cha mfumo wa pamoja wa kuratibu usalama. Lengo ni kuendeleza makubaliano ya amani ya mwezi Juni, lakini kutarajiwe nini hasa kwa siku hizi mbili za majadiliano?
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mkutano huu unaweza kuashiria mabadiliko katika mchakato wa amani kati ya Kinshasa na Kigali. Wajumbe kutoka DRC na Rwanda watakutana mjini Washington leo Jumanne na Jumatano kujaribu kuendeleza makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwezi Juni mwaka jana, kama sehemu ya kikao cha tatu cha mfumo wa pamoja wa kuratibu usalama, ulioanzishwa kama sehemu ya makubaliano ya amani yaliyotiwa saini Juni 27 nchini Marekani.
Pande hizii zilikutana mara ya mwisho katika muktadha huu mnamo Septemba 17 na 18, na kuamua kutekeleza Dhana ya Operesheni (CONOPS) kuanzia Oktoba 1. Waraka huu unazingatia vipengele vya uendeshaji na unaelezea hatua mbalimbali za operesheni ya kijeshi mara nyingi, na hivyo kuashiria mwanzo wa mapambano dhidi ya kundi la waasi wa Kihutu wa Rwanda (FDLR).
Kwa mantiki hiyo, Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC) lilituma ujumbe kwa waasi hao wa Rwanda, likiwataka wajisalimishe ama kwa FARDC au kwa MONUSCO.
Tathmini ya awamu ya kwanza ya mapambano dhidi ya FDLR
Lakini kulingana na ripoti za awali, FDLR bado haijajisalimisha, ama kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa au kwa jeshi la Kongo. Kwa hivyo mkutano wa siku mbili huko Washington utajikita katika kutathmini awamu hii ya kwanza ya mapambano dhidi ya kundi hili lenye silaha. Awamu ambayo uhamasishaji, upangaji, uratibu, na ushiriki wa taarifa za kijasusi utajadiliwa.
Kulingana na ratiba ya Operesheni, hatua inayofuata ni uendeshaji wa shughuli. Hii ni pamoja na hatua zinazolengwa dhidi ya FDLR, kuondoa kile kinachoitwa hatua za kujihami za Rwanda, na kukomesha shughuli za dharura na za kuvuka mpaka. Inabakia kuonekana iwapo pande husika zitaweza kupiga mbele pamoja, kuheshimu ahadi zao, licha ya mvutano wa maneno ulioshuhudiwa katika siku za hivi majuzi kati ya Kinshasa na Kigali.