Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesisitiza kuwa ni muhimu sana kudumisha usitishwaji vita uliyofanikishwa kwa juhudi kubwa hivi karibuni kati ya Israel na kundi la Kipalestina la Hamas huko Gaza.

Akifanya ziara rasmi Kuwait Jumatatu, Erdogan amekutana na Emi wa taifa hilo, Sheikh Meshal Al Ahmad Al Jaber Al Sabah, na walijadili uhusiano wa mataifa mawili pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa, kulingana na taarifa iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano ya Uturuki.

“Akisisitiza umuhimu mkubwa wa kudumisha usitishwaji vita uliyofanikishwa kwa juhudi kubwa Gaza, Rais Erdogan alisema kuwa suluhisho la mataifa mawili ni la lazima kwa amani ya kudumu, na alionyesha umuhimu wa msimamo wa pamoja wa nchi za Kiislamu kuhusu suala hili,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo pia ilieleza kuwa Erdogan “amesisitiza azma ya Uturuki katika kuhifadhi mshikamano wa kisiasa na uhuru wa mipaka wa Syria, na akaonyesha hamu ya kushirikiana na mataifa ya Kiarabu kwa pamoja katika kujenga mustakabali mzuri kwa watu wa Syria.”

Kuhusu uhusiano wa mataifa mawili, Erdogan alisema ushirikiano uliopo kati ya Uturuki na Kuwait katika nyanja za uwekezaji, nishati, biashara, na sekta ya ulinzi ni wa kimkakati.

“Rais Erdogan amesisitiza uwezekano wa kuimarisha zaidi uhusiano mzito wa mataifa hayo mawili,” iliongeza taarifa hiyo.

“Rais Erdogan pia alithamini juhudi za Kuwait za kuendeleza utulivu wa kikanda kama Mwenyekiti wa sasa wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba, na akasema kuwa Mkataba wa Biashara Huria, ambao bado unaendelea kujadiliwa kati ya Uturuki na Baraza la Ushirikiano la Ghuba, utakuza zaidi uhusiano wa kibiashara kati ya Uturuki na nchi rafiki za Ghuba,” iliongeza taarifa hiyo.

Uturuki na Kuwait wasaini makubaliano manne

Makubaliano manne yamesainiwa kati ya Uturuki na Kuwait mbele ya Erdogan na Sheikh Meshal.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *