#HABARI: Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza kuwa jumla ya wanafunzi 1,582,140 wa Darasa la Nne kutoka shule 20,517 nchini wanatarakiwa kufanya Mtihani wa upimaji wa Taifa wa Darasa la Nne (SFNA) utakaofanyika tarehe 22 na 23 Oktoba, 2025.
Akizungumza mapema leo Oktoba 21, 2025 jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Said Ally Mohamed, amesema kati ya watahiniwa hao, wavulana ni 764,290 (asilimia 48.31) na wasichana ni 817,850 (asilimia 51.69).
Ameeleza kuwa asilimia 93.27 ya wanafunzi watafanya mtihani kwa Kiswahili, huku asilimia 6.73 wakitumia Kiingereza, kutegemeana na lugha ya kufundishia inayotumika katika shule zao.
Aidha, jumla ya wanafunzi 5,750 wenye mahitaji maalum wamesajiliwa, wakiwemo wenye uoni hafifu, wasioona, wenye ulemavu wa kusikia, ulemavu wa akili, na ulemavu wa viungo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.