#HABARI: Chama Cha Mapinduzi CCM, kimeahidi kuendelea kuimarisha huduma za Kinga ndani ya Jamii, kupitia Programu kabambe ya Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii, ambao wamewezeshwa kwa mafunzo na kupewa vifaa kwa ajili ya kutoa huduma za msingi za afya pamoja na Elimu ya Afya ndani ya Jamii.

Mgombea Ubunge katika Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama akiwa katika Kata ya Kizuka katika Wilaya ya Songea Vijijini, amesema Mgombea wa nafasi ya Urais Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anayo nia njema ya kuimarisha huduma za Kinga kupitia wahudumu hao wa afya ngazi ya Jamii.

“Mgombea wa urais wetu pamoja na kuongeza ajira za watumishi wa afya, kupitia Serikali tayari alishaanzisha kundi la wahudumu maalum wanaojulikana kama Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii, na hapa tayari wameshachukuliwa na kupata mafunzo na kazi yao kubwa ni kupita nyumba kwa nyumba kutoa huduma za Afya kwa haraka”

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *