#HABARI: Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, leo hii inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya rufaa iliyokatwa na Clinton Damas maarufu kama Nyundo na wenzake watatu dhidi ya hukumu ya kifungo cha maisha gerezani.
Wakata rufaa hao tayari wamefikishwa ndani ya chumba cha Mahakama wakisubiri kusikiliza uamuzi huo ambapo wakata rufaa wengine ni Askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson maarufu Machuche, na Amin Lema anayejulikana kama Kindamba.
Ikumbukwe kuwa, Septemba 30, 2024, Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma iliwahukumu Nyundo na wenzake kifungo cha maisha gerezani baada ya kuwakuta na hatia ya makosa ya kubaka kwa kikundi na kumwingilia kinyume na maumbile binti mkazi wa Yombo, Dovya jijini Dar es Salaam, aliyetambulishwa Mahakamani kwa jina la XY.
Hukumu ya rufaa hiyo awali ilipangwa kutolewa Septemba 25, 2025, lakini iliahirishwa kutokana na sababu za dharura.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.