#HABARI: Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata jumla ya kilogramu10,763.94 za aina mbalimbali za dawa za kulevyapamoja na kilogramu 6,007 na lita 153 za kemikalibashirifu, huku watuhumiwa 89 wakikamatwakuhusiana na uhalifu huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema mafanikio hayoyametokana na operesheni zilizofanyika katika kipindicha mwezi Septemba na Oktoba 2025 katika maeneo mbalimbali nchini.
Kamishna Jenerali Lyimo amesema katika operesheni iliyofanyika eneo la Kariakoo, Dar es Salaam, Mamlaka ilikamata dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa kilogramu 40.32 zilizokuwa zimekaushwa na kufungwa kama viungo (spices) katika paketi 80 zenye maandishi ya “Dry Basil Leaves”. Dawa hizo zilikuwa zikisafirishwa kwenda nchini Canada na Italy kupitia makampuni yausafirishaji.
Ametaja waliokamatwa kuhusiana na dawa hizo kuwani Yusuphu S. Kibaha (35) na Mohamed H. Ramadhan (41), na uchunguzi wa awali umebaini dawa hizo ziliingizwa nchini kwa njia za kificho kutoka nchi jirani.
“Uchunguzi wetu umeonesha uwepo wa mtandao wausafirishaji wa mirungi unaotumia bodaboda na baadhiya mawakala wa kampuni za usafirishaji ili kurahisishakusafirisha dawa hizo bila kutiliwa shaka. Mtandao huu unaweza kuathiri taswira ya nchi yetu kimataifa, na sisi hatutalifumbia macho suala hili,” alionya Kamishna Jenerali Lyimo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.