#HABARI: Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa serikali yake itakwenda kusimamia na kukamilisha mradi wa miundombinu ya Barabara ya mabasi yaendayo haraka maarufu kama Mwendokasi, hiyo itafanyika ikiwa atachaguliwa kuiongoza nchi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Dkt. Samia ameyasema hayo akizungumza kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, ambapo amesisitiza kuwa utoaji wa huduma ya usafiri na usafirishaji kupitia miundombinu hizo zitakapokamilika, utajikita zaidi kwenye sekta binafsi.

Amewaahidi wakazi wa Dar es Salaam kuwa kuanzia Januari, 2026 kutakuwa na mageuzi makubwa ya utoaji wa huduma ya miundombinu ya Mwendokasi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *