
Makubaliano hayo ya kusitisha mapigano yaliyokuwa yamedumu kwa siku 11 baada ya msururu wa mashambulizi dhidi ya Hamas.
“Tunasisitiza ukosoaji wetu wa ukiukaji wa Israel huko Palestina hasa uharibifu uliofanywa katika Ukanda wa Gaza eneo ambalo si salama kwa maisha ya binadamu na ukiukaji unaoendelea wa usitishwaji wa mapigano,” alisema Shakh Tamim.
Tamko hili la emir wa Qatar linatolewa wakati ambapo Makamu wa Rais wa Marekani J.D Vance anatarajiwa kuwasili Israel leo kuzungumzia usitishwaji huo wa mapigano ambao umekuwa na mashaka katika siku chache zilizopita.
Wakati huo huo, Israel imesema imeutambua mwili wa mateka aliyerejeshwa na wanamgambo wa Hamas jana Jumatatu.
Ofisi ya waziri mkuu wa Israel imesema mabaki hayo ni ya Tal Chaimi mwenye umri wa miaka 41 aliyeuwawa mnamo Oktoba 7 mwaka 2023.
Chini ya makubaliano ya usitishwaji huo wa mapigano, Israel bado inasubiri Hamas wairejeshe miili ya mateka 15 waliofariki dunia. Miili 13 imerejeshwa tangu usitishwaji wa mapigano ulipoanza.