Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limepiga marufuku magari ya abiria kujaza mafuta wakati wakiwa na abiria ndani ya gari.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tabora, Mrakibu mwandamizi wa polisi SSP, Piter Magayane amewaonya madereva wa magari ya abiria wanaoingia vituo vya mafuta wakiwa na abiria ndani ya magari yao, na kusema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kukiuka agizo hilo.
Akizungumza wakati wa zoezi la utoaji wa elimu ya usalama barabarani, SSP Magayane amesena hatua hiyo inalenga kuzuia majanga yanayoweza kutokea katika vituo vya mafuta, ikiwemo milipuko inayoweza kusababisha vifo au majeraha makubwa kwa wananchi.
Amesema imebainika kuwa baadhi ya madereva wamekuwa wakipuuza tahadhari hizo kwa kisingizio cha haraka za safari, hali ambayo inaweka maisha ya abiria hatarini pamoja na wao wenyewe.
Aidha, SSP Magayane amewataka wamiliki wa magari kuhakikisha vyombo vyao vya usafiri vinakaguliwa na kuthibitishwa na maafisa wa LATRA kabla ya kuendelea na safari, akisema hatua hiyo itasaidia kuimarisha usalama barabarani.
#StarTvUpdate