df

Chanzo cha picha, Reuters

Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ali Khamenei, amesema kauli za Rais wa Marekani Donald Trump ni “mbaya na ni za uongo.”

Bw. Khamenei amesema: “Ina umuhimu gani kwa Marekani ikiwa Iran ina vinu vya nyuklia au la? Hatua hizi hazifai, si sahihi na ni za uonevu.”

Hotuba ya Khamenei imekuja baada ya takriban mwezi mmoja kutokuwepo mbele ya watu. Kauli zake amezitoa mbele ya mabingwa wa fani mbalimbali za michezo.

Ayatollah Khamenei amezitaja kauli za hivi karibuni za Trump katika safari yake ya Israel na Misri wakati wa kutia saini makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza kuwa ni upuuzi.

Trump alisema usitishaji vita huko Gaza haungewezekana bila kulipua vituo vya nyuklia vya Iran.

Khamenei amesema kuhusu Rais wa Marekani: “Mtu huyu alijaribu kuwatia moyo Wazayuni ili aonekane ana uwezo, kupitia tabia yake ya kuchukiza na uwongo mwingi kuhusu eneo hili na Iran. Lakini ikiwa ana uwezo basi aende kuwatuliza mamilioni ya watu wanaoandamana dhidi yake katika majimbo yote ya Marekani.”

Pia unaweza kusoma

Khamenei alikuwa akirejelea maandamano ya Jumamosi katika miji ya Marekani kupinga sera za Trump.

Akizungumza kuhusu vita vya siku 12 dhidi ya Israel, Kiongozi huyo amesema, “vikosi vyetu vya kijeshi na kambi zetu za kijeshi vilikuwa na makombora, yametumika na bado tunayo, na ikibidi yatatumika wakati mwingine.”

Rais wa Marekani, huku akijigamba kuhusu kulipua maeneo ya nyuklia ya Iran. Donald Trump amerejelea mara kwa mara kuhusu ulipuaji wa vituo vya nyuklia vya Iran kwa kutumia ndege ya kivita ya B-2 mwezi Julai mwaka huu na ametishia kuvishambulia tena ikibidi.

Hafla hiyo ya kuhitimu mafunzo ya wanafunzi kutoka vyuo vya kijeshi iliyofanyika mjini Tehran, imehudhuriwa pia na Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi, Mkuu wa Majeshi na Meja Jenerali Amir Hatami, Mkuu wa Jeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *