Mgombea ubunge wa Jimbo la Bukene, kupia Chama cha Mapinduzi (CCM), John Ruhende amesema endapo atachaguliwa atahakikisha anashi…Mgombea ubunge wa Jimbo la Bukene, kupia Chama cha Mapinduzi (CCM), John Ruhende amesema endapo atachaguliwa atahakikisha anashi…

Mgombea ubunge wa Jimbo la Bukene, kupia Chama cha Mapinduzi (CCM), John Ruhende amesema endapo atachaguliwa atahakikisha anashirikiana na wakazi wa eneo hilo kutafuta pamoja changamoto mbalimbali zinazolikubwa Jimbo hilo.

Luhende ambaye anaendelea na kampeni zake kwa kukutana na wakazi wa jimbo hilo amesema hayo Leo Jumanne Oktoba 21, 2025 wilayani Nzega, Tabora.

Kwa mujibu wa mgombea huyo, endapo wananchi hao watampa ridhaa, ataanza kuboresha mambo ya msingi ya kijamii ikiwamo upatikanaji wa maji, elimu na miundombinu.

Awali mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mkoa wa Tabora, Mohamed Hamdani amewataka wananchi hao kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura Oktoba 29 na kuchagua viiongozi wa chama hicho.

Wakizungukza katika mkutano huo, wakazi wa wilaya hiyo Shigamba Catherine Yunge na Malando Elius wamesema jimbo hilo linakabiliwa na kero tatu ikiwamo huduma za afya, upatikanaji wa maji safi na salama na barabara za kiwango cha lami kutoka Nzega kwenda Bukene hadi Mambali.

Shigamba Catherine Yunge na Malando Elias wakizungumza Katika magombea watakao pewa dhamani ya kuongoza kutatua kero hizo.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *