Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema hapati uchungu wala hajutii kutolewa mane…Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema hapati uchungu wala hajutii kutolewa mane…

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema hapati uchungu wala hajutii kutolewa maneno machafu na matusi kwa sababu ya kuwatumikia Watanzania.

Ameijenga hoja hiyo, akirejea historia za manabii akiwemo Yesu Kristo aliyekubali kusulubiwa msalabani kuwakomboa wananchi, vivyo hivyo kwa Mtume Muhammad aliyepigwa hadi kutolewa meno kwa ajili ya watu wake.

Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumanne Oktoba 21, 2025 alipozungumza na wananchi wa Kinondoni katika mkutano wake wa kampeni za urais, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

“Ndugu zangu mengine niachieni mimi, matusi niachieni mimi, nayabeba kwa niaba yenu, manabii wetu Bwana Yesu alisulubiwa kwa kukomboa watu kwa amri ya Mungu, lakini alikuwa anafanya kazi ya watu.

“Nabii Muhammad alipigwa hadi kung’olewa meno kwa kufanya kazi ya kukomboa watu kwa amri ya Mungu. Samia Suluhu aliapa kuitumikia Tanzania na ndicho ninachokifanya, niliapa kuilinda nchi na ndicho ninachokifanya,” amesema.

Amekwenda mbali zaidi na kueleza kila anachokifanya ikiwemo kutoa huduma za maji, umeme, elimu na afya analenga kuuheshimisha utu wa Mtanzania, hivyo haoni uchungu kubeba matusi kwa kazi hiyo.

“Kwa hiyo sina uchungu ndugu zangu, sina uchungu wa kubeba matusi yote yanayotolewa kwa sababu nafanya kazi hii, sina uchungu hata kidogo, wala sijutii,” amesema Samia.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *