Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka mitano ijayo, Serikali yake …Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka mitano ijayo, Serikali yake …

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka mitano ijayo, Serikali yake itajenga Barabara ya Bungu-Nyamisati, Kibiti-Mtumba na Rufiji-Mbwela.

Dkt Samia ametoa ahadi hiyo Jumatatu Oktoba 20, 2025 alipozungumza na wananchi wa Kibiti mkoani Pwani, katika mkutano wake wa kampeni za urais.

Ameahidi kujenga Barabara ya Bungu-Nyamisati, Kibiti-Mtumba, Rufiji-Mbwela na kuboresha barabara za ndani zikiwemo kilomi 42 za maeneo korofi ili zitumike misimu yote.

Dkt Samia amesema miradi ya maji 23 imekamilishwa wilayani humo na kuongeza upatikanaji wa huduma hiyo kutoka asilimia 47 hadi 74 na kwamba ataendelea kuboresha kuhakikisha wananchi wanapata maji zaidi Kibiti.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *