Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake katika miaka mitano ijayo, inatarajia kujenga zuio la mafuriko katika eneo la Rufiji mkoani Pwani, kudhibiti athari za mafuriko kwa wananchi.
Ujenzi wa zuio hilo la mafuriko kwa mujibu wa Dkt Samia, ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa mabwawa mawili ya Mbakimtuli na Ngorongo na skimu ya umwagiliaji itakayonufaisha hekta 13,000.
Dkt Samia ametoa ahadi hiyo leo, Jumatatu Oktoba 20, 2025 alipozungumza na wananchi wa Ikwiriri wilayani Rufiji katika Mkoa wa Pwani, katika mkutano wake wa kampeni za urais.
Amesema ujenzi huo wa zuio la mafuriko unatarajiwa kugharibu Sh245 bilioni na kwamba tayari mkandarasi ameshapatikana, tayari kuanza utekelezaji wa mradi huo.
Sambamba na mradi huo, amesema Serikali yake itajenga mabwawa mawili makubwa ambayo ni Mbakimtuli na Ngorongo, pia yakilenga kudhibiti mafuriko katika Bonde la Rufiji.
Ameeleza mradi huo utahusisha pia ujenzi wa skimu za umwagiliaji kwa ajili ya hekta 13,000 na barabara yenye urefu wa kilomita 90 na makaravati.
#StarTvUpdate