Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Watanzania kuwa, siku ya Uchaguzi…Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Watanzania kuwa, siku ya Uchaguzi…

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Watanzania kuwa, siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, hakutakuwa na maandamano zaidi ya kushuhudiwa wananchi wakienda kupiga kura.

Amelisisitiza hilo, akisema kwa kuwa yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu na ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, siku hiyo hakutashuhudiwa maandamano wala tishio lolote la kiusalama.

Dkt Samia ametoa hakikisho hilo, leo Jumanne Oktoba 21, 2025 alipozungumza katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Leader Club, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

“Ninaye ongeza hapa ndiye Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi hii. Nataka niwaambie maandamano yatakayokuwepo ni watu kwenda vituoni kupiga kura.

“Hakuna maandamano mengine yatakayokuwepo, hakuna tishio la kiusalama litakalokuwepo, anayesema ni Amiri Jeshi Mkuu wa nchi hii, niwaombe ndugu zangu, twendeni mkapige kura,” amesema.

Amesema kila mwananchi anapotoka kwenda kupiga kura anapaswa kuambatana na mwenzake aliyeandikishwa, kisha arudi nyumbani kwa usalama.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *