Mgombea wa Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kukamilisha ujenzi wa bwawa la Kidunda lenye gharama ya shilingi bilioni 336 ili kutatua changamoto ya maji katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
Amesema serikali pia imekamilisha upembuzi yakinifu wa mradi wa maji wa Mto Rufiji ambao utaanza kutekelezwa katika miaka mitano ijayo.
Dkt. Samia amesema ametoa ahadi hiyo leo Oktoba 21, 2025 Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam na kuongeza kuwa, miradi hiyo itahakikisha wananchi wanapata maji ya uhakika na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kumtua mama ndoo kichwani.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates