
Mufti wa Oman ametangaza himaya na uungaji mkono wake kikamilifu utayarifu wa Wayemen kukabiliana na utawala haramu wa Israel.
Katika ujumbe aliouandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, Sheikh Ahmed bin Hamad al-Khalili amepongeza utayarifu wa jeshi la Yemen wa kukabiliana na kuwaadhibu Wazayuni iwapo watakiuka ahadi yao na kukiuka usitishaji vita wa Gaza.
Mufti wa Oman ameandika: Asiyemshukuru kiumbe hatamshukuru Muumba. Lazima nitoe shukrani zangu zangu kwa Wayemeni mashujaa ambao wanafahamu uvunjaji wa ahadi na usaliti wa Wazayuni.
Natoa shukurani zangu za dhati kwa watu shupavu na mashujaa wa Yemen waliowatishia Wazayuni kwamba iwapo – baada ya kufikia mapatano na watu wa Gaza – watafanya usaliti, uvunjaji wa ahadii, watakuwa tayari kikamilifu kukabiliana na kusimama dhidi yao.
Mufti wa Oman amesisitiza kuwa: “Wayemeni walitishia kwamba iwapo Wazayuni watafanya makosa yoyote baada ya makubaliano ya usitishaji vita ya Ghaza, wako tayari kikamilifu kukabiliana nao. Mwenyezi Mungu awalipe mema na awasaidie.” Huko nyuma Mufti wa Oman, Sheikh Ahmed Al-Khalili, amewahi pia kutoa shukrani na pongezi zake kwa misimamo ya uungaji mkono ya Yemen kwa wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, ambao wamekuwa wakikabiliwa na vita vya mauaji ya halaiki, mzingiro, njaa na kunyimwa haki na adui wa Israel kwa takriban miaka miwili.
Hivi karibuni pia Mufti Mkuu Oman, Sheikh Ahmed bin Hamad Al-Khalili, alisisitiza kuwa, leo hii majeshi ya madola dhalimu na ya kibeberu duniani yameinamisha vichwa vyao mbele ya Yemen na akayataka mataifa yanayotaka kuwa huru duniani, kuiga mfano wa Yemen katika kukabiliana na maadui wa mataifa yao.