Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Movies, Shamsa Ford amesema kitu kikubwa kilichopitwa na wakati kwa mastaa ni kuigiza maisha kwa sababu hata hizo pesa za kuigizia hakuna.
Akizungumza na Mwananchi, Shamsa Ford amesema kama kuna staa anahangaika na kuigiza maisha atakuwa anachelewa sana kufanya vitu vyake maishani na mwisho wake atapotelea kwenye kuigiza siku zote.

“Mambo ya kuigiza na kufeki maisha yalipitwa na wakati, tuigize katika michezo yetu tu na si katika maisha halisi, maana zamani hata hela za kuigizia zilikuwapo ila sio sasa,” amesema Shamsa Ford.

Shamsa Ford aliwahi kutamba na filamu ya Chausiku na pia kwenye tamthilia mbalimbali ikiwamo ‘Fundi’ iliyoandaliwa na msanii wa filamu Duma na pia amefunga ndoa na muigizaji mwezake Hussein Lugendo ‘Mlilo’ mwaka 2023.