McLaren tayari wamebeba taji la timu bora kwa mwaka wa pili mfululizo na dereva wao Muastralia Oscar Piastri anaongoza jedwali la dereva bora akiwa na pengo na pointi 14 dhidi ya dereva mwenza wa McLaren Muingereza Lando Norris.

Timu hiyo ilishinda mara ya mwisho taji la dereva bora ikiwa na Lewis Hamilton mwaka wa 2008 na hawajawahi kubeba ubingwa wa madereva wawili katika msimu mmoja tangu 1998.

Verstappen, anayewinda taji la tano mfululizo, yuko nafasi ya tatu na pengo la pointi 40, lakini amepunguza mwanya huo kutoka pointi 104 mwishoni mwa Agosti kwa kushinda mara tatu katika raundi nne za mwisho. Bado kuna raundi tano zilizobaki.

“Nadhani kulingana na mwenendo wa leo (Jumapili) ni mbio za kutia moyo kiasi kwa sababu nadhani bila kulazimika kupigana na Charles (Leclerc), ambalo hakika lilikuwa pambano lenyewe la kuburudisha, nadhani Lando alikuwa na kasi ya kushinda,” Stella aliwaambia waandishi wa habari.

Stella amesisitiza mtizamo wake kuwa Verstappen bado yuko kwenye mapambano ya ubingwa.

“Kwangu mimi hakuna siri, tunajua kuwa Max anapokuwa na nyenzo za kushinda, anakuwa mshindani mkali sana kushinda. Kwa hiyo, haibadilishi uelewa wetu wa hali ilivyo, haibadilishi tunachofanya,” aliongeza.

“Lazima tuendelee kuongeza kasi yetu na kuendelea kupata matokeo mazuri kila wikiendi.

Mashindano yajayo, raundi ya 20 kati ya msimu wa mizunguko 24, yatakuwa Mexico City wikiendi hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *