
Chanzo cha picha, Getty Images
Mchezaji wa Sporting Morten Hjulmand, 26, ameibuka kama shabaha kuu ya Manchester United kuimarisha safu yao ya kiungo na klabu hiyo ya Ligi ya Premia ina matumaini ya kumpata Mdenmark huyo kwa takriban £50m. (Teamtalk)
Wamiliki wa Fulham wamemwambia kocha mkuu Marco Silva kuhusu nia yao ya kutaka kuongeza mkataba wake, ambao una kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 15. (The Athletic)
Barcelona na Real Madrid wanamfuatilia kwa karibu beki wa kati wa England Marc Guehi, 25, ambaye hataongeza mkataba wake na Crystal Palace baada ya mwisho wa msimu huu. (Fichajes)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Porto Mhispania Samu Omorodion, 21, yuko kwenye orodha ya ya wanaolengwa na Tottenham . (TBR Football)
Arsenal wanaendelea na juhudi zao za kumuongezea mkataba mlinzi wa Uholanzi Jurrien Timber, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 na The Gunners sasa wakiwasiliana moja kwa moja. (GiveMeSport)
Beki wa pembeni wa Everton wa Ukraine Vitalii Mykolenko, 26, anavivutia vilabu vya Uhispania na Italia. (Footmercato)

Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa pembeni wa Strasbourg Guela Doue, 23, amekuwa akitazamwa na vilabu vya Ligi ya Premia, Chelsea, Aston Villa, Brighton na Brentford, ingawa timu hiyo ya Ufaransa inaweza kudai ada ya uhamisho ya zaidi ya £26m kwa mlinzi huyo wa Ivory Coast. ( Caught offside)
Leeds wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Maccabi Tel Aviv kutoka Mali Issouf Sissokho, 23, mwezi Januari. (Africafoot)
Aston Villa inamfuatilia kwa karibu winga wa Real Sociedad na Japan Takefusa Kubo, 24, ambaye ameamua kutaka kuondoka La Liga mwezi Januari. (Fichajes)