Hata hivyo Trump amesisitiza kuwa anatoa nafasi kwa kundi hilo kuheshimu makubaliano hayo, na ameitoa kauli hiyo wakati akimtuma Jumanne nchini Israel Makamu wake JD Vance ili kuungana na wajumbe wawili wakuu wa Marekani Steve Witkoff na Jared Kushner kujadili hali inayoendelea huko Mashariki ya Kati baada ya ghasia za hivi karibuni.

Makubaliano hayo ya kusitisha vita Gaza  yaliyosimamiwa na Trump na yaliyoanza kutekelezwa Oktoba 10, yalikuwa hatarini kuvunjika baada ya wanajeshi wawili wa Israel kuuawa kusini mwa Gaza, na kupelekea Israel kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya Hamas na kusababisha vifo vya Wapalestina wapatao 45.

    

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *