Rais aliyeko madarakani kwa sasa Yoweri Museveni atatafuta kuongeza muda wa utawala wake hadi kufikia karibu nusu karne katika uchaguzi huo.

Kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa 2021, mpinzani mkuu wa Museveni anatarajiwa kuwa Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine.

Wine anasema Museveni alishinda uchaguzi uliopita kutokana na wizi wa kura na vitisho kwa wapiga kura, madai yanayokanushwa na maafisa wa chama tawala cha NRM, wanaosema Museveni alishinda kihalali kutokana na uungwaji mkono aliokuwa nao.

Akiwa rais wa nne Afrika aliyehudumu kwa muda mrefu, Museveni na serikali yake wameifanyia mageuzi katiba ya Uganda na kuondoa ukomo wa umri na kuwa madarakani. Amekuwa madarakani tangu 1986.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *