
Vyanzo na mashahidi wanaripoti milipuko ya mapema asubuhi karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum, ambao umekuwa umepangwa kufunguliwa tena leo Jumatano.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Msururu wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yalikumba vitongoji katika mji mkuu wa Sudan, ikiwa ni pamoja na karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khartoum, usiku wa kuamkia Jumatano siku ambayo ilikuwa imepangwa kufunguliwa tena kwa uwanja huo, kulingana na shirika la habari la AFP na vyombo vya habari vya Sudan.
Mashahidi walmeliambia shirika la habari la AFP kuwa walisikia ndege zisizo na rubani katikati na kusini mwa Khartoum mapema siku ya Jumanne. Wimbi la milipuko limeripotiwa karibu na uwanja wa ndege kati ya saa 10 alfajiri na 12 asubuhi.
Uwanja wa ndege umefungwa tangu mapigano yalipoanza mwezi Aprili 2023 kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), ambavyo viliharibu vibaya miundombinu.
Gazeti la kila siku la Sudan la Rakoba News, likinukuu mashahidi, limeripoti zaidi ya milipuko minane ndani na karibu na uwanja wa ndege. Gazeti hilo lilihusisha RSF kwa mashambulizi hayo ambapo inadaiwa kuwa “ndege zisizo na rubani,” zilitumiwa kwa mashambulizi hayo.
Gazeti la Sudan Tribune lenye makao yake mjini Paris pia limeripoti kuhusu shambulio hilo la ndege zisizo na rubani, likinukuu vyanzo vya usalama na mashahidi walioona “moshi mwingi… ukipanda kutoka eneo la uwanja wa ndege.”
Chanzo cha usalama cha eneo hilo kimeliambia chombo hicho kuwa jeshi la Sudan liliangusha baadhi ya ndege zisizo na rubani.
Hakuna kundi lililodai kuhusika mara moja na shambulio hilo, na hakuna maelezo yaliyopatikana juu ya idadi ya majeruhi au uharibifu.