
Taarifa hiyo imesema viongozi wa Ulaya watakutana baadae wiki hii katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya, katika mfumo wa “muungano wa wenye nia” kwa nchi zinazoiunga mkono Ukraine. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atahudhuria mkutano huo mjini London siku ya Ijumaa.
Rais Trump pamoja na kiongozi mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, wanapanga kukutana katika mji mkuu wa Hungary, Budapest.
Hungary ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya kujihami ya NATO, ila imekuwa na mahusiano mazuri na Urusi katika kipindi chote cha vita vya Ukraine.