Xi

Chanzo cha picha, Reuters

Vyombo vingi vikubwa vya habari duniani vimeripoti namna rais wa China anavyoongoza nchi yake kuelekea kuwa imara na ubora kimataifa kwa gharama ya Marekani chini ya uongozi wa Donald Trump.

Lakini makala hii itaangalia hilo na mapendekezo yaliyoelekezwa kwa Trump ya kumbwaga Rais wa Urusi, Vladimir Putin, kabla ya mkutano wao wa Budapest.

Gazeti la Uingereza The Guardian na makala yenye kichwa cha habari: “Xi Jinping anajiandaa kwa mapambano na Donald Trump katika vita ambavyo vitatoa mshindi mmoja tu”, kuna mengi ya kuyatizama.

Mwandishi wa makala hiyo, Simon Tisdall anaulezea mkutano unaotarajiwa mwishoni mwa mwezi kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Xi Jinping. Alibainisha kwamba mbio ya uongozi wa dunia kati ya Marekani na China katika karne ya 21 inaenda vizuri zaidi kwa upande wa Xi, “ukisaidiwa na makosa ya kimkakati ya Trump.”

Tisdall alifuatilia mjadala mkali kuhusu malengo ya China na aliashiria kuwa Xi anadhamiria kuimarisha udhibiti wa usafirishaji wa rasilimali muhimu, hatua inayofanana na umonopolio na yenye madhara kwa nchi zinazokabiliana naye. Rasilimali hizi, alisema Tisdall, ni muhimu kwa utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki na silaha za kisasa, ikiwemo makombora, ndege za kivita, meli zenye nyuklia na droni, jambo linalochochea Magharibi kutafuta mbadala.

Tisdall anaamini kwamba marufuku ya China, ikiwa yataanza mwezi ujao, yataathiri usambazaji wa silaha wa Magharibi kwa Ukraine, na China pia inakusudia kudhibiti utengenezaji wa rasilimali hizi nje ya nchi yake, ikifuatia mfano wa Marekani. Alisema: “Hii inaleta Beijing kwenye mgongano na Washington katika njia ambayo hii ya mwisho ilianza miaka kadhaa iliyopita kutumia biashara kama silaha ya kisiasa.”

Tisdall alibaini kwamba Trump alikasirika wakati China ilitangaza hatua hizi, akitishia kutoza ushuru wa asilimia 100 na kufuta mkutano, lakini alilazimika kurudi nyuma kutokana na hofu sokoni. Vikwazo vya pande zote bado vinaendelea, na hofu ya mzozo wa kiuchumi duniani inaongezeka.

Tisdall alionya: “Trump, kama kawaida, hufanya mambo bila mpango na hana wazo la kinachofanyika, tofauti na Xi Jinping, ambaye anaonekana amedhamiria kuishughulikia Marekani ikiwa itasisitiza vita vya kibiashara vya kina.”

Tisdall pia anaamini Beijing inatambua kwamba sera za ‘Marekani kwanza’ za Trump zimewapunguzia hadhi washirika wake, na kutengeneza pengo ambalo China inaweza kulitumia kama fursa. “Wakati Marekani inashuka, China inapaa chini ya uongozi wa Xi Jinping, ambaye anaonekana kudhamiria kuweka nchi yake mbele ya dunia.”

Trump lazima “amtulize” Putin kabla ya kilele cha Budapest

a

Chanzo cha picha, Shutterstock

Gazeti la Marekani The New York Post, ambalo liliandika kuhusu mkutano unaotarajiwa kati ya Trump na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, wiki chache zijazo, kwa matumaini ya kumaliza vita nchini Ukraine.

Gazeti hilo linasema Trump anapaswa “kujifunza kutoka kwa diplomasia yake ya Mashariki ya Kati na kuuweka mkutano huu chini ya masharti yake mwenyewe.”

Gazeti hilo lilipendekeza Trump iipe Ukraine makombora ya Marekani ya mbali ya Tomahawk, na kuongeza idadi hiyo iwapo inahitajika, pamoja na kutangaza ulimwenguni kwamba vikwazo vya pili vitatekelezwa dhidi ya Urusi ikiwa mkutano wa Budapest hautazaa matunda ya haraka ya kusisitishwa kwa vita.

New York Post ilionya kujirudia kwa hali kama ya mkutano wa Alaska mwaka uliopita, wakati Putin hakutekeleza kile kilichokuwa kimeahidiwa na diplomasia yake. Gazeti hilo lilionyesha kwamba makombora ya Tomahawk (na labda Barracuda pia) yangewezesha Wa-Ukraine kuharibu miundombinu ya mafuta na gesi ya Urusi, ambayo ni chanzo kikuu cha kifedha cha vita.

Gazeti linasema hatua inayofuata ni tangazo rasmi la vikwazo vya pili, ambavyo vitachukua gharama kubwa kwa China kwa kuunga mkono Urusi, ikiwa Putin hatakubali Kusitisha vita kwenye mkutano huo Budapest. New York Post inaamini Trump “ana kadi zote za mchezo, na mwenzake wa Urusi atajifanya mjinga ikiwa atalazimisha Trump kutumia kadi zote.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *