
Uamuzi wa Zelensky ni baada ya kushindwa wiki iliyopita kumshawishi rais wa Marekani Donald Trump kumpatia makombora ya masafa marefu ya Tomahawk.
Katika hotuba yake ya video Jumatatu usiku, Zelensky amesema alipokuwa Washington alizungumza na watengenezaji wa silaha hizo na wakaonyesha utayari wa kushirikiana na Ukraine lakini akasisitiza kuwa upatikanaji wa mifumo hiyo ya ulinzi wa anga si jambo rahisi, lakini ni moja ya hakikisho la usalama itakayosaidia kwa muda mrefu.
Hata hivyo Zelensky alisifu mkutano wake na Trump licha ya kauli ya rais huyo wa Marekani kusema hapo jana kuwa haamini ikiwa Ukraine itashinda vita dhidi ya Urusi, ingawa hajaondoa kabisa uwezekano huo.