BARUAN MUHUZA AWAPA NENO MASHABIKI YANGA: “Nawaomba wapunguze presha kwa wachezaji na viongozi”
Gwiji wa habari nchini @baruan_muhuza amewasihi mashabiki wa Yanga kuacha kuwatia presha viongozi na wachezaji kuelekea mechi yao ya mkondo wa pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers.
Meneja huyo Mwandamizi wa Azam Media, amesema Silver Striker ni timu ndogo sana hata kama inacheza vizuri na anaamini Yanga itavuka kwenda hatua ya makundi bila shida yoyote.
Ally Kamwe atia utani kwa Singida BS na Azam FC.
#YangaSC #Yanga