DRFA YAFANYA JAMBO KUELEKEA MABINGWA WA MIKOA (WANAWAKE)

DRFA YAFANYA JAMBO KUELEKEA MABINGWA WA MIKOA (WANAWAKE)

Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kimekabidhi shillingi 500,000/ kwa timu za wanawake za Mbagala United, Masala Princess na Ilala Queens kuelekea katika Ligi ya Mabingwa wa Mikoa soka la wanawake ambayo itarajiwa kuanza Novemba 3, 2025 mkoani Mwanza.

Mwenyekiti wa chama hicho, Lameck Nyambaya ameeleza malengo ya fedha hizo huku akiwaomba wadau wengine pia wajitokeze kuziunga mkono timu hizo kutoka Dar es Salaam.

Ligi ya Mabingwa wa Mikoa kwa wanawake ndiyo itakayotoa timu zitakazopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara.

#DRFA #WomenFootball #Nyambaya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *