Chuki dhidi ya rais wa hivi sasa wa Marekani imekuwa jambo la kawaida kwa waandamanaji wanaomiminika mitaani kumpinga Trump katika majimbo mbalimbali na hivi sasa imegeuka kuwa nembo ya mshikamano mpya huko Marekani.

Gazeti la The Guardian la Uingereza limeandika habari hiyo hiyo na kuongeza kwa kusema: Wakati baadhi ya Warepublican wa Marekani walitaraji kuwa maandamano makubwa yaliyobebwa na kaulimbiui ya “Hatutaki Wafalme” (No Kings) yangegeuka kuwa vurugu siku ya Jumamosi, ukweli ni kuwa maandamano hayo yanaendelea hadi hivi sasa na hakuna vurugu zinazotokea kwani waandamanaji wanaunganishwa na hasira zao kwa Donald Trump.

Kwa mujibu wa gazeti hilo la nchini Uingereza, mamilioni ya Wamarekani wameingia mitaani katika miji mbalimbali ya Marekani, kuanzia New York hadi Austin mpaka Oakland na St. Augustino kuonesha jinsi wanavyochukizwa mno na sera za kimabavu na kibeberu za Donald Trump. Tofauti na kilivyotarajia chama tawala cha Republican, maandamano hayo yanafanyika kwa amani, shauku, furaha pamoja na ucheshi na hamasa za kisiasa.

Siku chache kabla ya kufanyika maandamano hayo, baadhi ya watu mashuhuri katika chama tawala cha Republican huko Marekani, akiwemo Spika wa Bunge Mike Johnson, walijaribu kuonesha kuwa mikutano hiyo ni kichocheo cha vurugu nchini Marekani. Johnson aliyaita maandamano hayo kuwa “mikusanyiko ya kuipinga Marekani” na alidai kwamba washiriki walikuwa ni kutoka kwa makundi ya “Marxist, anti-FA, socialist na pro-Hamas” lakini njama hizo za kueneza chuki dhidi ya wageni na hasa Waislamu zimeshindwa kufua dafu mbele ya mamilioni ya Wamarekani wanaochukizwa na siasa mbovu na za kibeberu za Trump.

Mbunge wa Minnesota, Tom Emmer aliyaita maandamano hayo kuwa ni matokeo ya mrengo wa kigaidi wa Chama cha Democratic, naye Seneta Roger Marshall alifikia hata kudai kuwepo uwezekano wa kutumiwa askari wa Gadi ya Taifa kukandamiza maandamano hayo, lakini njama hizo pia zimefeli na maandamano dhidi ya Trump yanaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *