#HABARI: Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, John Heche, amesafirishwa hadi Tarime na Jeshi la Polisi baada ya kukamatwa leo asubuhi.

Gaston Garubindi, wakili mkurugenzi wa Sheria wa Chama cha CHADEMA, amethibitisha hilo na kuongeza kuwa kama chama wanajipanga kwa ajili ya mawakili waliopo Mkoa wa Mara na wengine kutoka Mwanza kwa ajili ya kutoa huduma za kisheria.

Heche alikamatwa asubuhi ya leo Oktoba 22, 2025 akiwa njiani kuelekea kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu katika Mahakama ya Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *