#HABARI: Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam Oktoba leo 22, 2025 siku ya Jumatano inatarajia kutoa uamuzi juu ya mapingamizi manne ikiwemo kupinga uhalali wa shahidi wa tatu wa Jamhuri yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Bwana Tundu Lissu ambaye anakabiliwa na kesi ya uhaini.
Mapingamizi mengine ni kuiomba Mahakama kutopokea vielelezo vya video na ‘flash disc’ ambazo ziliwasilishwa na shahidi wa tatu kama sehemu ya ushadhidi wake akiwa ni mtaalamu wa picha na video kutoka Jeshi la Polisi Makao Makuu.
Uamuzi huo unatolewa kwa sasa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru akiwa na majaji wenzake wawili na tayari mtuhumiwa Tundu Lissu amefikishwa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Wafuasi na viongozi wa ngazi ya juu wa CHADEMA akiwemo Katibu Mkuu Bwana John Mnyika tayari amefika Mahakamani pia.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.