#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amewaonya wananchi na makundi yote katika jamii kuepuka vitendo vyovyote vya vurugu, uchochezi au uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Sendiga amesema maandalizi ya uchaguzi huo yanaendelea vizuri huku hali ya usalama ikiwa imetulia katika mkoa mzima wa Manyara.
Amesema hadi sasa hakuna taarifa yoyote kuhusu mtu au kikundi kinachopanga kufanya vurugu, na kusisitiza kuwa utulivu na amani ni jukumu la kila mmoja.
“Tunawataka wananchi wote wawe watulivu, waende wakapige kura kwa amani na baada ya kupiga kura warudi majumbani mwao kusubiri matokeo. Amani na utulivu ni vitu vya lazima, haviepukiki,” amesema Sendiga.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania