#HABARI: Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felister Mdemu amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mbeya kufanya kazi kwa bidii na kujituma katika kuwahudumia wananchi katika vituo vyao vya kazi.
Mdemu ameyasema hayo, wakati akikabidhi pikipiki kumi na mbili (12) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya lengo kuu ikiwa ni kuwasaidia Maafisa hao hasa wanaoishi vijijini kuzitumia kuwafikia wananchi na kuwahudumia kwa wakati.
Mdemu amesema lengo kuu la kuwapatia pikipiki hizo ni kutambua thamani ya mchango wao kiutendaji pamoja na kuwarahisishia kazi wakati wa ufuatiliaji na utatuzi wa changamoto za kijamii.
“Tunaomba mkawajibike ipasavyo kwani kwa sasa mmerahisishiwa utendaji kazi wenu kwa kupewa vyombo vya usafiri (Pikipiki) ili kuwafikia wananchi katika maeneo yao na kuwahudumia.” amesema Mdemu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania