#HABARI: Takribani watu 63 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa kwa ajali iliyohususha magari manne yakiwemo mabasi mawili, lori na gari dogo aina ya Toyota Land Cruiser, katika Barabara ya Kampala na Mji wa Gulu nchini Uganda.
Kwa mujibu wa ripoti ya awali ya polisi, chanzo cha ajali hiyo iliyotokea Jumatano asubuhi katika Kijiji cha Kitaleba ni mabasi mawili kugongana na kusababisha magari hayo mengine mawili kuanguka kwenye barabara kuu nchini Uganda mapema na kuua watu 63 na kujeruhi wengine kadhaa huku idadi ya vifo ikielezwa kuwa inaweza kuongezeka kutokana na baadhi ya abiria kujeruhiwa vibaya.
“Inaelezwa kuwa basi lililokuwa likitoka Kampala lilikuwa likilipita lori na basi jingine lililokuwa likielekea Kampala lilikuwa likiipita gari ndogo ya Toyota Land Cruiser, lakini lilishindwa kufanya hivyo kwani tayari basi lililokuwa likitoka Kampala lilikuwa limekaribia,’’ taarifa ya polisi imeeleza.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.