Mamlaka ya Iran imetangaza siku ya Jumatano, Oktoba 22, “kuachiliwa kwa masharti” kwa raia wa Iran, Mahdih Esfandiari, aliyekamatwa nchini Ufaransa mwezi Februari kwa kutetea ugaidi kwenye mitandao ya kijamii.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Ufaransa haikuthibitisha mara moja kuachiliwa kwa raia huyo. Katika taarifa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran “imekaribisha uamuzi wa jaji wa Ufaransa wa kumwachilia Bi. Esfandiari chini ya usimamizi wa mahakama.” “Itaendeleza juhudi zake” hadi “atakapoweza kurejea nchini.”

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Paris imelithibitishiashirika la habari la AFP kuachiliwa kwa Mahdih Esfandiari chini ya usimamizi wa mahakama, uamuzi uliochukuliwa na Mahakama ya Jinai ya Paris, dhidi ya hoja ya mwendesha mashtaka wa umma. Usimamizi wa mahakama unamtaka kuripoti katika kituo cha polisi na kumkataza kuondoka nchini hadi kesi itakaposikilizwa kwa kuzingatia uhalali wake, iliyopangwa Januari 13 hadi 16, 2026.

Alikamatwa Ufaransa kwa kuendeleza ugaidi

Mamlaka ya Iran iliomba mara kwa mara kuachiliwa kwa mwanafunzi huyo anayeishi Lyon, ambaye alikamatwa nchini Ufaransa mwezi Februari mwaka jana kwa, kulingana na mahakama ya Ufaransa, kuendeleza ugaidi kwenye mitandao ya kijamii. Alirusha machapisho dhidi ya Israeli kwenye mitandaoya kijamii.

Kufuatia kuachiliwa na mamlaka ya Iran kwa mateka wa Ufaransa mwenye asili ya Ujerumani Lennart Monterlos, Tehran ilionyesha matumaini ya kuachiliwa kwa karibu kwa wanandoa Cécile Kohler na Jacques Paris, ambao walikuwa wakishikiliwa kiholela na katika mazingira magumu, kulingana na Ufaransa. Kwa kubadilishana, raia wa Iran,Mahdih Esfandiari, aliyekamatwa nchini Ufaransa alipaswa kuachiliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *