Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt Samia S…Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia S…

Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi bilioni 527.751 kwa ajili ya kuhudumia jumla ya miradi 13 ya kitaifa kwa jumla ya kilomita 612.4, madaraja manne na mizani minne ya Kizengi miwili na Mizani ya Mkolye katika mkoa wa Tabora.

Mkoa wa Tabora una mtandao wa Barabara wa kilometa 2188.09, katika mtandao huo, Barabara kuu ni kilometa 1077.12 na Barabara za mkoa ni kilometa 1073.37 na kilomita 37.6 ni za Wilaya. Aidha jumla ya Kilomita 803.66 za Barabara kuu ni za kiwango cha lami na kilomita 273.46 ni za changarawe, kwa Barabara za mkoa kilomita 44.75 ni za lami na kilomita 1,028.62 ni za changarawe na kilomita 4 ni za kiwango cha lami na kilomita 33.6 ni za kiwango cha changarawe.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 22 Octoba 2025 na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tabora Mhandisi Raphael Mlimaji ofisini kwake Mjini Tabora wakati akizungumzia miaka minne ya Rais Samia tangu aingie madarakani ambapo ameitaja miradi 7 iliyokamilika yenye thamani ya shilingi bilioni 488.152 pamoja na madaraja manne sawa na asilimia 92.5 huku miradi mingine 6 yenye thamani ya shilingi bilioni 39.598 sawa na asilimia 7.5 ikiwa inaendelea na hatua mbalimbali za ujenzi.

Ameitaja miradi ya Kitaifa iliyokamilika kuwa ni Pamoja na ujenzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Tabora ambao umefikia asilimia 97 unaotekelezwa na Mkandarasi Beijing Construction Engineering Group kwa shilingi bilioni 27.943 chini ya Mhandisi mshauri Khatibu&Alami Consulting Engineers Offshore S.A.L, ujenzi wa Barabara ya Nyahua – Chaya yenye urefu wa kilomita 85.4 na madaraja mawili (Nyahua na Kizengi) iliyojengwa na mkandarasi CHICO kwa gharama ya shilingi Bilioni 117.939 pamoja na ujenzi wa Barabara ya Usesula – Komanga yenye urefu wa kilomita 108 iliyojengwa na mkandarasi Jiangxi Geo Engineering Group chini ya Mhandisi mshauri Leah International Ltd iliyojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 158.825

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *